KULIKUWA NA SABABU GANI?

Picha hii uilipigwa juzi huko igunga mkoanin Tabora ambapo Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Ismail Aden Rage alionekana kwenye jukwa la kampeni akiwa na Bastora kama inaooneka.UC blog tunajiuliza ?je kulikuwa na ulazima gani kwa Mbunge huyu kupanda na bastola kwenye jukwaa tena akiwa amezungukwa na wananchi ambao walifika pale kwa ajili ya kusikiliza kampeni?
Hata hivyo WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, amewaagiza polisi kumhoji kuhusu hatua yake ya kupanda jukwaani na bastola kiunoni. Taarifa iliyopatikana na kuthibitishwa na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ambao hawakupenda kutajwa, ilisema polisi wameagizwa kuwa baada ya kumhoji mbunge huyo, wawasilishe ripoti hiyo kwake haraka iwezekanavyo.
Miongoni mwa mambo ambayo polisi wameelekezwa kumhoji Rage ni pamoja na endapo anaimiliki bastola hiyo kihalali. Mambo mengine ni sababu alizoeleza wakati anaiomba bastola hiyo na hatua yake ya kwenda nayo kwenye mkutano wa hadhara.

Comments
Post a Comment