NONDO ZAENDELEA MKOANI MBEYA..


Bwana Elia Daudi Mwalonde mkazi wa Uyole akiwa hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya wodi namba 1 baada ya kupigwa nondo.

Matukio ya upigaji Nondo jijini Mbeya yameibuka kwa kasi mpya ambapo watu kadhaa wamekwisha poteza maisha na wengine wamesababishia ulemavu wa kudumu.
Baadhi ya maeneo ambayo wananchi wamekuwa wakipigwa Nondo ndani ya jiji hili ni Ilemi, Isanga, mabatini, Air Port, Uyole, Mwanjelwa na Soweto.
Kutokana na kuibuka kwa vitendo hivyo Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi ametangaza vita dhidi ya wanaojihusisha na vitendo hivyo na kusema kuwa doria imeanza rasmi ili kuwabaini wahusika.
Wakati huohuo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za siri ambazo zitafanikisha kukamatwa kwa watu hao wanaojihusisha na vitendo vya upigaji Nondo.Mdau wa UC Blog bwana Wigan Mponela kutoka Mbeya ameiambia Blog hii kuwa hali ni mbaya kiasi kwamba wanalazimika kurudi majumbani mapema ili kujiepusha na hali hiyo katika jiji hilo la mbeya.(picha kwa hisani ya mbeya yetu)

Comments

Popular Posts